Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP), unaotekelzwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kampasi ya Mwanza.

Mradi huo unaohusisha ujenzi wa jengo la taaluma, utawala mabweni mawili na jengo la taaluma ya ngozi unafadhiliwa na Benki ya dunia kwa gharama ya Sh billioni 37.

“Nafurahi kusikia kwamba mkandarasi utamaliza kazi ndani ya mwaka huu ingawaje kwa muda huu uko nyuma kwa miezi miwili. Ongeza kasi ukamilishe kwa wakati na kazi iendelee kuwa bora uendelee kupata ‘tenda’ zingine hapa kupitia ushindani maana mradi huu unatekelezwa kwa awamu,” alisema.

Wakati huohuo ameelekeza uongozi wa DIT kuzingatia suala la wanafunzi kubadilishana ujuzi na taasisi zingine za elimu nje ya Tanzania mahiri katika taaluma ya ngozi ili kupata wataalam wabobezi wa kutosha katika tasnia hiyo.

Amesema serikali imekua ikiingia mikataba ya makubalino (MoU) ya kubadilishana ujuzi na taasisi mbalimbali za elimu ya juu, ndani na nje ya Afrika, akasisitiza DIT kutumia fursa hiyo, kuendelea kupeleka wakufunzi na wanafunzi katika vyuo hivyo kwa makubaliano .

Kaimu Mkurugezi wa Kampuni ya Confix and engineering Limited, ambo ni wakandarasi wa mradi huo, Mhandisi Allan Magoma, amekiri mradi kuwa nyuma kwa muda kwa miezi miwili, lakini kazi inafanyika usiku na mchana ili kuzipa pengo.

Alisema sababu za kuwa nyuma ni mvua zilizonyesha mfululizo wakati wa kuabza ujenzi pamoja na kubadili michoro.

“Ujenzi wa jengo hili la taaluma pamoja na mabweni yote utakamilika mwezi Oktoba, na wa jengo la utawala utakamilika mwezi Novemba,” alisema.

Akijibu swali kuhusu matokeo tarajiwa ya mradi, Mkuu wa Kampasi Albert Mmari, amesema usajili wa wanafunzi utaongezeka takribani mara 10, kutoka 200 wa sasa hadi 2,000 na kwamba kutokana na mindombinu hiyo wanatarajia wahitimu bora na wenye ujuzi katika Tasnia ya ngozi.

Elimu kwa vitendo nayo itaboreshwa kwani mradi kwa ujumla wake (awamu ya